Rafiki ya Mama

mother's friend

Nayafungua macho yangu na kukutana na giza. Kiza kingi mno. Najaribu kuyafikicha macho yangu Lakini nagundua kuwa nimefungwa. Lo! Itakuwaje?Macho yangu yanazoea kile kiza kwani bado Mna mwanga unaoingia mle chumbani. Nyumba ya msonge niliyomo ndani. Najiambia. Ninapotazama juu nahakikisha fikra yangu ya kuwa nipo kwenye nyumba ya msonge. Nyota mle angani zimetapakaa kwelikweli na nahisi kama kwamba zinanichekea kwa hali yangu hii. Nasongeza miguu. Nazo pia zimefungwa. Najaribu kutoa ukemi.Ah! Nmebanwa mdomo.

Naanza kuvuta taswira nikiwa mle chumbani, Licha ya kichwa changu kuuma kana kwamba nagongelewa misumari. Nakumbuka jinsi ambavyo wanaume wawili wanene walivyoniteka na kunieka ndani ya gari. Licha ya Mimi kupigana nao, walinishinda nguvu. Najichekea nikikumbuka jinsi ambavyo mimi na mwili wangu mdogo nilivyokuwa nikipigana na wale majibaba. Najiona kama kifaranga Cha kuku ambacho kinajaribu kujinasua kutoka kwenye meno ya mauti ya mwewe. Ninapoingizwa mle ndani, najaribu kuzua vurugu na hapo nilipokea Kofi moja ambalo liliyavimbisha mashavu yangu na kunifanya nitokwe na machozi. Huku nikilia na kupiga yowe basi nikazibwa mdomo wangu. Vilio vikaishia kuwa kwikwi. Nikiwa mle garini, nikajiuliza. Itakuwa ni wale watu wateka watoto? Lakini mbona Mimi? Tena familia yangu ni ya wastani. Si hawa wateka watoto wanawateka watoto ambao kwao ni mabwanyenye Ili kupata Hela? Au ni wale wateka watoto Ili wawatoe kafara? Kafara hapana. Najibembeleza huku kijasho chembamba kikinitiririka kwapani na usoni. wametumwa? Kutumwa haiwezekani. Sina ugomvi na mtu. Nashindwa kupata majibu ya maswali yangu. Gari linaendeshwa kwa mwendo wa dakika thelathini hivi kisha linasimama. Natolewa mle ndani na kupelekwa chumbani. Mle chumbani wananirusha kama gunia LA mahindi na kunifanya nizimie kwa kukosa nguvu. Hali hii imetokana na Kilio na pia fikra nyingi.

Nakaa nikijililia huku nikiwaza jinsi wazazi wangu walivyo waliponikosa nyumbani. Tena Leo ni siku ya mikosi tu! Najiambia. Asubuhi niliamkia kelele za mama kisa nimevunja bakuli yake anayoipenda. Tena mama kasema Leo nisitoke nje. Na nikiondoka niwe mwangalifu. Lakini akasisitiza nisiondoke. Nikaona tu ni Yale maneno ya mama Ili kunifanya nikae nyumbani. Rafiki yangu alipokuja kunitembelea na kunieleza kuwa Leo amenijia Ili tuende tukatazame kikosi kimoja pale mtaani Cha densi, nikahisi sababu kubwa ya mama kuishauri nisitoke nje. Kikosi hiki nakipenda sana kwa sababu kinanipa furaha na hata tamaa ya kukua mcheza densi. Kumbe mama alijua kikosi hicho kitakua Tena “ live”, ndio maana akasema nisiondoke. Nikamwambia rafiki yangu kuwa tutaambatana na yeye Lakini nitatoka mapema Ili niwahi nyumbani. Tulipofika, nikazubailia ile “ performance” na pia masaa nazo zikaanza kupita. Sekunde ikawa dakika, dakika ikawa lisaa limoja. Lisaa baaada ya lisaa. Nilipoangalia saa yangu nikashtuka. “ jamani, masaa yaani ni kama yamekimbizwa. Mama atawahi mbele yangu. Hivi Mimi nitaondoka’ Nikamuita Martha na kumueleza kuwa nitaweza kuondoka. Martha akanizidikisha na kunifikisha kwenye kichochoro kimoja hatari pale mjini. Mwanzo nilikuwa nimemkatalia swahibu wangu.”We Martha hujui kuwa hiki kichochoro hatari sana. Watu wenye hadhi zao wanabakwa seuze sisi vinyangarika? La Mimi siwezi kuyahatarisha maisha yangu. Naomba tu tupite njia ya kawaida.” Martha anaagua kicheko ambacho kinanishtua. “ Mna Nini? Kitu gani hapo Cha kuchekesha? Yaani Mimi nakueleza masahibu ya kupita kwenye kichochoro hichi nawe wacheka?” hasira imenipanda. Sijielewi Tena.” Poa moto dada. Hivi sikujua kuwa wewe mwoga hivo. Mimi nipo. Tena tu wawili. Nani atatushinda?” “ sipendelei kabisa. Mbona tusipite njia ya kawaida?” “ We nawe, tukipita njia ya kawaida basi mama atawahi nyumbani mbele yako.” Nakumbuka maneno ya mama kuwa nisiondoke mle nyumbani. Akiwahi mbele yangu, itakuwa kesi. Tena kesi kubwa. Itabidi tu nipite kwenye kile kichochoro. Sikujua kilichokuwa kikinisuburi mle. Nikaagana na rafiki yangu kisha nikaamua kupita kwenye kile kichochoro. Kufika katikati nikahisi nikama nafuatwa. Nikakaza mwendo. Lakini nilipojaribu kukimbia ndipo nilipotekwa na ndio sababu niko katika hali hii.

Kosa kubwa ikiwa ni kukosa kumsikiliza mama yangu. Subiri kidogo. Hivi Ina maana mama alijua kuwa hiki kitandeka au vipi? Au mama ana adui? Au ilikuwa dhana yake? Nitajua tu. Najikalia mle gizani huku nikisubiri hata mwokozi. Mara ghafla nahisi sauti. Hatimaye Kuna mtu yuaja mle chumbani. Au ni askari? Ina maana mama Kesha peleka ripoti polisi? Najaribu kufungua mdomo Lakini umezibwa. Mlango unafunguliwa. Sauti za kiatu zinanikaribia. Aliyeingia ni mwanamke. Licha ya Giza Lakini harufu ya marashi nainusa. Hii harufu nikama naikumbuka. Nimeihisi kwa muda mrefu. Lakini kumbukumbu za mwenye marashi hazijileti Kichwani. Haidhuru nitamjua tu. Anaingia na koroboi mkononi. Mwanga wa ile koroboi hauniruhusu kumuona aliyeingia. Kisha naisikia sauti. Sauti ambayo inanishtua na kuniletea kumbukumbu.

“ si sauti hii naifahamu? Au naisikia vingine. La haiwezi. Amefikaje huku? Tena mbona aniteke nyara? Rafiki mkubwa wa mama? La. Akili zangu, mwili wangu na kila kitu kinakataa. Haiwezi. “ vipi mwanangu?” salamu hiyo inafuatwa na kicheko cha dharau. Najihakikishia. Kweli huyu ndiye rafiki mkubwa wa mama na si mwengine ila mamake Martha! Ngoja. Ina maana pia Martha yupo katika hili suala? Au? Jamani mimi nitachizi nikiendelea vivi hivi. “ Mama Martha? Unafanya nini hapa? “ najibiwa kwa kofi. Kofi nzito ambalo linaniacha machozi yakinitiririka. “ nyamaza!” anafoka. “ lakini mama…( hilo ndilo jina nilikuwa namuita, pia Martha alimuita vivyo hivyo mamangu), si wewe na mama ni marafiki wakubwa? Imekuwaje unanifanya hivi” “ nimesema nyamaza. Mimi na mamako ati marafiki wakubwa?” kicheko cha dharau tena.” Najuta la sijuti. Sasa hivi nahisi kuwa moyo wangu utakuwa huru. Kitendo ambacho mamako mzazi alinifanyia siwezi kumsamehe na ntafurahia kuona kitoto ambacho kilichukua furaha yangu, nikikimaliza mwenyewe.” “ una maana gani? furaha yako? Niliichukua aje?” “ naona mamako hajakwambia, mimi na mamako tulikuwa marafiki wazuri pale shuleni. Tulikuwa marafiki wa chanda na pete. Palitokea kuwa mamako aliambulia ujauzito.

Aliye mpa ujauzito huo alikuwa ni mwanamume mmoja niliyempenda sana. Licha ya mamako kujua kuwa mimi na huyo mwanamume tuko pamoja, alienda na kushiriki ngono na yeye. Mama yako aliniomba msamaha na nikaahidi kumsamehe, ila kwa jambo moja. Aitoe ile mimba. Mama yako akakataa katakata kuwa hawezi kuitoa ile mimba na juu ya hapo, akaamua kuolewa na mpenzi wangu. Nikajiamulia moyoni nitajifanya nimemsamehe lakini huyo mtoto aliyebeba, nitamtesea yeye ili ajue uchungu nilio nao.” “ yaani ina maana miaka hii yote umebeba donda moyoni? Tena ukajifanya kuwa rafiki na mama yangu?” “ ndio. Najua mamako yuakupenda sana. Na sasa mahali yupo hayupo sawa. Anapitia mateso juu yako. Na kitu kingine, hawezi nishuku mimi.” Simu inaita. Anaiangalia na kuubana mdomo wangu aliokuwa ameubanua. “ halloo, vipi rafiki yangu?…nipo salama…mbona hivo? Mna nini? Ati nani? Mwanangu amepotea?…jamani anaweza kuwa kaenda wapi?… Umetaarifu polisi?…usijali atapatikana tu. Na naja hivi sasa” kauli ya mwisho hainikalii vizuri. Ina maana anaenda nyumbani kwetu, ampe mamangu bega alilie, na ndiye mhusika mkuu?, Haitawezekana. Anamaliza kuongea na kunitoa kile kitambaa alichonibania.

“ Umeona? Naenda nyumbani kwenu nikamliwaze mama yako. Hiyo ni baada ya kukumaliza na mwili wako kuutelekeza barabarani. Adhabu hiyo itaumiza mamako na pia itanipea furaha.” Siamini masikio yangu. Ananiua mimi. Kwa vijisababu ambavyo havinihusu? Ulimwengu huu. Namwamgalia na kumueleza kuwa kuniua mimi hakutampa furaha hata kidogo. Haya ni mambo yako na mama yangu na baba yangu. Mbona hamkukaa mkayasuluhisha?, Mimi nitakuwa nakufa bure. Iyo itakupa furaha gani? Furaha gani kuua mtoto kisa unata kufanya kisasi cha mamake kuvunjwa moyo kwako? Mimi niliyekutambua na kukujua kama mama yangu wa pili? Leo hii nakuona vitofauti. Tena sana. Mbona unataka kumpa mtoto wako shida? Urafiki tulionao na Martha unataka kuuharibu tu kwa ubinafsi wako?, Unadhani Martha atakupenda anavyokupenda atakapojuwa kuwa umemuua rafiki yake wa karibu? Unadhani mambo yatakuwa sawa? Maswali hayo yote nampa yeye huku machozi yakinitiririka. Ninapomwangalia, naona macho yake yamekua mekundu. Ananisogelea na kunikumbatia. Anaanza kuniomba msamaha. Ila namwambia kuwa mwenye kuombwa msamaha ni mamangu alfu wasikizane na waishi vizuri.” Ngoja. Mbona unamchukia mama hivi na waliachana na baba miaka mingi iliyopita?” ananiangalia na kuniambia kuwa ni kiapo alikiapa baada ya mamangu kumsaliti kuwa liwalo na liwe mtoto huyo atamuua.
SOMO: Wakati mwingine tujifunze kuyaweka mambo yetu nyuma. Ukiamua kumsamehe mtu basi msamehe. Usikae karibu yake ukiongoja fursa ili ulipize kisasi. Na kama utalipiza kisasi, basi iwe kati yenu. Msije mkaingiza watu wengine ambao mambo yenu hayawahusu.

Story Shared by:

Faith Ndinda

Leave a Reply