Rafiki ya Mama
Nayafungua macho yangu na kukutana na giza. Kiza kingi mno. Najaribu kuyafikicha macho yangu Lakini nagundua kuwa nimefungwa. Lo! Itakuwaje?Macho yangu yanazoea kile kiza kwani bado Mna mwanga unaoingia mle chumbani. Nyumba ya msonge niliyomo ndani. Najiambia. Ninapotazama juu nahakikisha fikra yangu ya kuwa nipo kwenye nyumba ya msonge. Nyota mle angani zimetapakaa kwelikweli na…