Hapo zamani za kale palikuwa na mzee mmoja aitwae Kanyawi ambaye alihamia kijiji cha Ntenga kutoka Usambaani. Mzee huyu alikuwa anapenda sana kunywa pombe na hata alipomaliza fedha zake zote aliamua kuweka rehani chochote alichonacho. Hakika mzee huyu alikuwa kero sana kwa familia yake kwani kila aliyekopwa alifika nyumbani kwake na kudai deni lao. Kutokana na heshima waliyokuwa nayo watoto wake na mke wake; walilazimika kulipa madeni mara kwa mara. Ilifikia wakati ambapo mke na watoto wote ilibidi kubuni miradi mbalimbali ili waweze kulipa madeni na kusomeshana. Mtoto mkubwa aliyeitwa Mwasu alibuni mradi wa kufuga nyuki na hivyo kuchonga mizinga ya nyuki mizuri sana pale kijijini.
Siku moja kama ilivyokuwa kawaida ya Mzee Kanyawi; alikopa tena pombe ya dengelua yenye thamani ya shilingi elfu tatu. Baada ya kudaiwa alimuambia aliyemkopesha kuwa afike nyumbani kwake kesho yake ili ampe fedha zake. Keshoye yule aliyemkopesha alimpigia mzee Kanyawi simu kuwa yupo njiani kwenda kuchukua fedha zake.
Mzee kanyawi kusikia hivyo aliangalia juu ya mti uliokuwa karibu na nyumba yake na kuona mzinga mpya wa nyuki ambao bado haujaingliwa na nyuki na kumwambia mke wake kuwa kuna watu wanakuja kumuua na hivyo ataingia ndani ya ule mzinga na afungiwe mle ili wale wanaomdai wasimuone. Kutokana na upendo mkubwa kwa mumewe alikubali ombi lile na kumfungia mumewe ndani ya mzinga wa nyuki. Punde si punde Yule mzee Mwasu alifika na kuulizia alipokuwa mzee Kanyawi. Mke wake alimtetea na kusema kasafiri ghafla hadi wiki ijayo. Mzee Mwasu alisononeka sana na kuamua kuchukua ule mzinga uliokuwa juu bila kujua kuwa yule mzee alikuwa ndani yake na kuondoka nao hadi nyumbani kwake. Alipofika kwake Mzee Mwasu aliulizwa na mkewe iwapo alifanikiwa kupata fedha zile na kumwambiwa kuwa hakumkuta lakini aliamua kuchukua mzinga wake mpya ili waupasue na kupata kuni za kupikia kwani yule mzee sio mlipaji. Mzee Mwasu alimtaka kijana wake wa kazi achukue shoka na kupasua ule mzinga ili wapate kuni za kupikia chakula. Hadi hapo yule mzee Kanyawi alikuwa kimya ndani ya mzinga akisubiri jioni ili atoke na kurudi kwake.
Kijana yule wa “miraba minne” alichuka shoka na kulishushia kewnye mzinga ule na “ghafla” damu zilitapakaa kila mahali. Walipoangalia vizuri waliona kuwa ni yule mzee Kanyawi kapasuliiwa kichwa. AMA KWELI KIAMA CHA MKOPAJI KILIMTOA ROHO BILA KUOMBA MAJI.
XXXXXXX MWISHO XXXXXX
Hadithi hii imetungwa na Sekiete Mtana. Darasa la sita Shule ya Msingi Ushindi.

Click on a star to rate this story.

Average rating 0 / 5. Vote count: 0

No votes so far! Be the first to rate this post.